KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Tuesday, April 19, 2016

JAHAZI YAWANYAKUA AISHA VUVUZELA, ZUBEDA MLAMALI



KUNDI la muziki wa taarab la Jahazi, limeendelea kujiimarisha baada ya kuwanyakua waimbaji wawili nyota, Aisha Othman 'Vuvuzela' na Zubeda Mlamali.

Aisha, anatokea kundi la Modern Taradance wakati Zubeda alikuwa mwimbaji wa kundi la East African Melody.

Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf amethibitisha kujiunga kwa nyota hao wawili katika kundi lake hilo.

Waimbaji hao walianza kuonekana kwenye maonyesho ya Jahazi, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati kundi hilo lilipofanya onyesho kwenye ukumbi wa Travertine, Magomeni, Dar es Salaam.

"Ni kweli nimeamua kuwachukua Aisha na Zubeda ili kuongeza nguvu katika kundi langu. Kikubwa ni kwamba nimezingatia uwezo mkubwa wa waimbaji hawa.

"Naweza kusema uwezo wao ndio umenishawishi kuwachukua na kuanzia sasa, wataendelea kuwepo Jahazi na Mungu akipenda katika albamu ijayo, naweza kuwapa nyimbo mpya,"alisema Mzee Yussuf.

Hata hivyo, Mzee alisema kupewa nyimbo kwa wasanii hao kutategemea kujituma kwao, nidhamu nzuri na utendaji mzuri wa kazi.

No comments:

Post a Comment